Wajibu Na Shuruti Za Hajj
Imefasiriwa na Ummu 'Abdil-Wahaab
Allah
Amewaamrisha waja Wake kuitekeleza ibada ya Hijja kwenye Nyumba Tukufu,
na kuwalipa malipo mema kutokana na ibada hiyo. Yeyote mwenye
kuitekeleza Hijja kwenye Nyumba hiyo (Ka'abah) na akawa hakumkaribia
mkewe kwa matamanio ya nafsi yake, wala hakutenda dhambi yoyote, basi
atatoka kwenye ibada hiyo hali ya kuwa hana dhambi yoyote mfano wake ni
kama mtoto mchanga ambaye ndio kwanza amezaliwa na mama yake. Hijja
iliyokubaliwa (Al-Hajj Al-Mabruur) malipo yake si chochote ila ni Pepo.
Enyi watu! Muogopeni Allah na jitahidini kuutekeleza wajibu wa Hijja, ambao Allah Amekuamrisheni juu yenu. Allah amesema:
((إِنَّ أَوَّلَ بَيْتٍ وُضِعَ لِلنَّاسِ لَلَّذِي بِبَكَّةَ مُبَارَكًا وَهُدًى لِّلْعَالَمِينَ ))
((
فِيهِ آيَاتٌ بَيِّنَاتٌ مَّقَامُ إِبْرَاهِيمَ وَمَن دَخَلَهُ كَانَ
آمِنًا وَلِلّهِ عَلَى النَّاسِ حِجُّ الْبَيْتِ مَنِ اسْتَطَاعَ إِلَيْهِ
سَبِيلاً وَمَن كَفَرَ فَإِنَّ الله غَنِيٌّ عَنِ الْعَالَمِينَ))
((Hakika Nyumba ya kwanza waliowekewa watu kwa ibada ni ile iliyoko Bakka, iliyobarikiwa na yenye uongofu kwa walimwengu wote))
((Ndani yake
zipo Ishara zilizo wazi - masimamio ya Ibraahiym, na mwenye kuingia humo
anakuwa katika amani. Na kwa ajili ya Allah imewajibikia watu wahiji
kwenye Nyumba hiyo, kwa yule awezae njia ya kwendea. Na atakayekanusha
basi Allah si mhitaji kwa walimwengu)) [Al-'Imraan: 96-97]
Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:
((Uislaam
ni kushuhudia ya kwamba Hapana Mola anaestahiki kuabudiwa kwa haki ila
Allah na Muhammad ni Mjumbe wa Allah, kusimamisha sala, kutoa Zakaah,
kufunga mwezi wa Ramadhaan, na kuhiji kwenye Nyumba Tukufu kwa mwenye
uwezo)) [Muslim]
Mtume
(Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema Uislaam umejengeka
kutokana na hizi nguzo tano na endapo yoyote miongoni mwa nguzo hizi
tano ikikosekana basi, Uislaam hautimii. ‘Umar Ibnul-Khattaab (Radhiya
Allahu 'anhu) amesema; "Nilikuwa karibu
nitume wajumbe katika miji kuchunguza wale walio na uwezo wa kufanya
Hijjah lakini hawafanyi, ili niwaamrishe walipe kodi, hao si Waislamu,
hao si Waislamu".
Wajibu
wa Hijja umethibitishwa katika Kitabu cha Allah na Sunnah za Mjumbe wa
Allah (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na vile vile kwenye
makubaliano ya wanavyuoni wa Kiislaam. Mtu yeyote anaepinga wajibu huu,
huyo hana dini, na yeyote anaeacha wajibu huu eti kwa sababu ya
kutojali, japo kuwa mtu huyo anaamini, huwa yupo kwenye ukingo wa
ukafiri.
Baada ya kubainisha (kuainisha) Wajibu wa Hijja, Allah Anasema
((
فِيهِ آيَاتٌ بَيِّنَاتٌ مَّقَامُ إِبْرَاهِيمَ وَمَن دَخَلَهُ كَانَ
آمِنًا وَلِلّهِ عَلَى النَّاسِ حِجُّ الْبَيْتِ مَنِ اسْتَطَاعَ إِلَيْهِ
سَبِيلاً وَمَن كَفَرَ فَإِنَّ الله غَنِيٌّ عَنِ الْعَالَمِينَ))
((Ndani
yake zipo Ishara zilizo wazi - masimamio ya Ibraahiym, na mwenye
kuingia humo anakuwa katika amani. Na kwa ajili ya Allah imewajibikia
watu wahiji kwenye Nyumba hiyo, kwa yule awezae njia ya kwendea. Na
atakaye kanusha basi Allah si mhitaji kwa walimwengu)) [Al-'Imraan: 97]
Huwaje
kwa Muislamu akajihisi kasalimika hali ya kuwa kaipuuza Hijja na ilhali
ana uwezo wa kuitekeleza kiafya na kifedha, na anafahamu kuwa Hijja ni
wajibu, na ni moja miongoni mwa nguzo za Kiislaamu?
Huwaje
kwa Muislaamu kujizuia fedha kuzitumia kwa ajili ya Hijja, na hali ya
kuwa anazitumia fedha hizo kwa mambo ya anasa za kidunia?
Huwaje kwa Muislaamu akajihifadhi kutokana na uchovu wa Hijja, lakini anajitahidi kwenye mambo (ya kipuuzi) ya kidunia?
Huwaje mtu akawa mvivu katika kuitekeleza Hijja, hali ya kuwa ibada hii imeamrishwa mara moja tu katika uhai wake?
Huwaje mtu akaakhirisha kuitekeza Hijja, na ilhali hajui kuwa uhai wake utafikia angalau siku moja ijayo au la?
Hivyo,
Muogopeni Allah enyi waja, na timizeni wajibu wa Hijja ambao
umeamrishwa juu yenu, tekelezeni kwa dhati ya kumpenda Yeye, yakubalini
maamrisho Yake na fanyeni hima na hamu ya kumtii Yeye, ikiwa nyinyi ni
waumini wa kweli. Allah Anasema:
((وَمَا
كَانَ لِمُؤْمِنٍ وَلَا مُؤْمِنَةٍ إِذَا قَضَى اللَّهُ وَرَسُولُهُ
أَمْرًا أَن يَكُونَ لَهُمُ الْخِيَرَةُ مِنْ أَمْرِهِمْ وَمَن يَعْصِ
اللَّهَ وَرَسُولَهُ فَقَدْ ضَلَّ ضَلَالًا مُّبِينًا))
((Haiwi
kwa Muumini mwanamume wala Muumini mwanamke kuwa na khiari katika
jambo, Allah na Mtume Wake wanapokata shauri katika jambo lao. Na mwenye
kumuasi Allah na Mtume Wake basi hakika amepotea upotofu ulio wazi)) [al-Ahzaab:36]
Ikiwa
Muumini ataitekeleza ibada ya Hijja mara moja tu baada ya kufikia
balegh, basi itatosheleza na atakuwa ameutimiza msingi muhimu wa
Uislaamu. Hatotakiwa tena kutekeleza Hijja wala Umrah baada ya hapo,
isipokuwa ikiwa kama aliweka nadhiri ya kutekeleza moja kati yake, basi
atawajibika kuitekeleza nadhiri yake kama tulivyofundishwa na Mtume wetu
(Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) katika Hadiyth ifuatayo:
Kutoka
kwa mama wa waumini 'Aaishah (Radhiya Allahu 'anhaa kwamba Mtume
(Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Yeyote
atakayeweka nadhiri ya kumtii Allah basi amtii. Na yeyote atakayeweka
nadhiri kumuasi Allah basi asimuasi)) [Al-Bukhaariy]
No comments:
Post a Comment