FAIDA NA MATUMIZI YA MAFUTA YA MISKI
FAIDA NA MATUMIZI YA MISK:
Hali yake ina ujoto na uyabisi katika daraja la pili. Ina ladha na
harufu tofauti na mafuta mengine mazuri. Inatokana na mnyama anaeitwa
kwa kiarabu AL GHAZALI. Namna ya kutofautisha Misk halisi na feki ni kwa
kuonja ladha
yake na kunusa harufu yake. Pia njia nyingine ni kwa kusomea aya za
Ruqya kwenye misk halisi halafu ajipake mwenye matatizo ya majini,
italeta athari na kama ni misk feki haiwezi kuleta athari. Vile vile
misk feki haiwezi kutibu maradhi ya kimwili kama vile maradhi ya ngozi.
MATUMIZI YA MISK KATIKA TIBA:
1) UBONGO NA MISHIPA YA FAHAMU: Kuna tiba iitwayo kitaalamu
Aromatherapy. Maana yake ni kupata dawa kwa njia ya kunusa au kupata
harufu yake kama vile kufukiza udi, misk huchangamsha ubongo na kuipa
nguvu mishipa ya fahamu. Utakuwa unanusa misk mara kwa mara au upate
mvuke wake. Kwa kupata mvuke wake chukua bakuli halafu uweke ndani yake
maji ya moto yaliyochemka halafu uweke ndani yake matone kadhaa ya misk.
Sogeza bakuli karibu ya usoni mwako ili upate kuvuta mvuke wake. Hali
kama hii, mvuke wa misk utakuingia kupitia puani au mdomoni. Tiba hii
inaitwa Aromatherapy. Ni nzuri kwa watu wenye kifafa, dege dege, kuumwa
na kichwa, kizunguzungu, kutopata usingizi na kuondosha kichefuchefu.
Pia huongeza kumbu kumbu.
2) RHEUMATISM: Ni dawa ya kuondosha maumivu ya miguu, ganzi na
viungo. Ule ujoto wa misk huondosha maumivu ya mishipa, viungo, miguu,
mgongo na kiuno.
3) MZUNGUKO WA DAMU: Husaidia mzunguko wa damu na kuondosha presha.
4)Kwa mwanamke inazidisha hisia na hamu ya tendo la ndoa.
5) HUONDOSHA HARUFU MBAYA: Kwa kuondosha harufu mbaya makwapani au miguuni, jipake misk.
6) FANGASI SEHEMU ZA SIRI: Huondosha sehemu za siri mwashowasho, mapele na harufu mbaya.
MATUMIZI YA MISK KWA KUMDHOOFISHA AU KUMFUKUZA JINI WA MAHABA:
Kwanza kabisa misk isomewe aya za Ruqya, kisha mgonjwa mwenyewe ajipake kila siku asubuhi na jioni viungo 32 vya mwili wake.
-Tundu mbili za pua.
-Tundu mbili za masikio.
-Kope mbili za macho.
-Mdomoni kama vile mfano wa lipstiki.
-Chuchu mbili (mwanamke anaenyonyesha asipake)
-Sehemu za siri mbele na nyuma.
-Kitovuni.
-Mbele mwa kucha zote za vidole 20 vya mikono na miguu.
TAHADHARI:
Ikiwa misk ni feki faida zote hapo juu za tiba haziwezi kupatikana.
No comments:
Post a Comment