LISHE YA KUONGEZA KINGA MWILINI NA CD4
Virusi vya ukimwi ( V.V.U. ) hudhoofisha nguvu za mwili
kujikinga na maradhi nyemelezi. Mgonjwa hushambuliwa na
maradhi kwa sababu kinga mwilini imepungua. Lishe ya kuongeza
CD4 husaidia kuongeza kinga mwilini na kupunguza makali ya
ukimwi.
ZINGATIA;
Siyo watu wote wenye maambukizi ya ukimwi wanalazimika kuanza
kutumia lishe ya kuongeza CD4 na kupunguza makali ya ukimwi.
Utaanza tu kutumia kwa kutegemea hali ya afya yako, idadi ya
chembechembe za CD4..
LISHE NA DAWA ZA KUONGEZA CD4 NI NINI ?
Ni dawa zenye uwezo wa kupunguza makali ya V.V.U
mwilini.Huongeza kinga mwilini na kumpa mgonjwa nafuu kwa kumpa
nguvu ya kufanya shughuli zake kama kawaida.
Ikiwa kinga itapungua sana na kuanza kushambuliwa mara kwa mara na
maradhi nyemelezi, unashauriwa uanze kutumia lishe ya CD4.
LISHE YA KUONGEZA KINGA MWILINI.
Kwa ajili ya kuongeza kinga mwilini tumia moja ya fomula nne za hapa chini:
CD4 Fomula 1
Vitu vinavyohitajika:
Mbegu za figili (unga) - kijiko kimoja cha chakula.
Haba Soda (unga) - kijiko kimoja cha chakula.
Kitunguu thaumu (unga) - kijiko kimoja cha chakula.
Asali - lita moja
Sufa - kijiko kimoja cha chakula.
Mdalasini (unga) - kijiko kimoja cha chakula.
Matayarisho: Vitu vyote hivyo vichanganywe pamoja hadi viwe juisi.
Matumizi: Kunywa vijiko vitatu vya chakula kutwa mara tatu.
CD4 Additive Fomula 2:
Vitu vinavyohitajika:
Karoti 2
Ndizi mbivu 2
Pilipili mboga 2
Chumvi kidogo
Ndimu 1
Nanasi robo kilo
Njegere robo kilo
Kunde mbichi robo kilo
Papai bichi 1
Karanga robo kilo
Embe kubwa 1
Parachichi 1
Matayarisho: Vitu vyote hivyo visagwe pamoja hadi viwe juisi.
Matumizi: Kunywa glass moja kutwa mara mbili.
CD4 Additive Fomula 3
Vitu vinavyohitajika:
Karoti iliyosagwa robo kilo.
Kitunguu thaumu (unga) robo kilo.
Mdalasini wa unga robo kilo.
Tangawizi ya unga robo kilo.
Majani ya Alovera matatu (yasagwe).
Asali lita moja.
Limau 2
Matayarisho: Ongeza maji lita mbili na uache kwa muda wa masaa 8 kisha chuja na uhifadhi
kwenye friji.
Matumizi:
Kikombe cha kahawa kutwa mara 4 kwa muda wa mwezi mmoja.
CD4 Additive Fomula 4
Vitu vinavyohitajika:
Tende 1kg.
Kitunguu thaumu robo kilo.
Maziwa halisi 1 lita.
Uwatu vijiko vikubwa vinne.
Mdalsini (unga) vijiko vikubwa vinne.
Tangawizi ya unga vijiko vikubwa vinne.
Haba Soda ya unga vijiko vikubwa vinne.
Matayarisho:
Saga tende na maziwa kwa pamoja kisha changanya vitu vingine na weka jikoni na kuvipika
pamoja hadi viive.
Matumizi:
Kula vijiko viwili vikubwa (vya chakula) mara tatu kwa siku kwa muda wa miezi mitatu.
Zingatia: Baadhi ya vitu vilivyotajwa hapo juu vinapatikana kwenye maduka ya dawa za
Kisunnah na Kiarabu, hivyo ni muhimu kuvipata kutoka kwenye maduka halisi yanayouza vitu
hivyo.
No comments:
Post a Comment