MDALASINI NA ASALI
Asali
inafahamika vema Duniani kote kama mojawapo ya silaha ya kiajabu
katika kupigana na magonjwa na matatizo yatokanayo na uzee.
Sasa hivi, utafiti mpya umeonyesha kwamba uwezo wa asali unaweza
kuongezwa maradufu kama itachanganywa na mdalasini wa kawaida.
Uchunguzi wa kina ufanywao kwa wiki na jarida la World News wa Tiba,
wataalamu wa madawa yatokanayo na mimea pamoja na kijarida cha afya na
lishe, imeonekana kwamba kuna dazani nyingi za umuhimu wa asali na
mdalasini pamoja na michanganyiko {dawa} ya kusisimua iletayo afya
bora.
Kama ifuatayo:
1. Ugonjwa wa Viungo/Maumivu na Uvimbe {ARTHRITIS}.
Wataalamu wa lishe wanapendekeza kuchukua kwa kutumia mchanganyiko wa
sehemu moja ya asali pamoja na sehemu mbli za maji vuguvugu na kijiko
kimoja {cha chai} chenye mdalasini - na kuchua sehemu zilizoathirika.
Nafuu hupatikana katika muda wa dakika moja.
Vinginevyo tengeneza chai-kikombe kimoja chenye maji moto, weka vijiko
vya chakula -viwili vya asali kwa kijiko cha chai cha mdalasini.
Kunywa asubuhi na jioni ili kuondoa maumivu.
Katika tafiti iliyofanyika hivi karibuni na chuo kikuu kimoja huko
Copenhagen, madaktari waliwapa wagonjwa 200, {syrup} mchanganyiko wa
kijiko kimoja 'cha chai' cha asali na kimoja cha mdalasini kila
asubuhi kabla ya kifungua kinywa. Asilimia 73% yao waliripoti nafuu
kubwa ya maumivu yao na ongezeko katika kufanya shughuli kama kujongea
na kutembea vyema.
2. Kukatika kwa nywele {HAIR LOSS}
Asali ikishachanganywa na mdalasini pamoja na mafuta vuguvugu ya olive,
hutoa kichocheo maridhawa cha kuotesha nywele kinachotumika katika
dawa ya Dork. Mchanganyiko huo vuguvugu unapakwa kwa kusugua kichwani
na kuachwa kwa dakika 15.
3. Ukungu wa miguuni {FUNGUS}
Changanya kijiko kikubwa cha mezani cha asali, vijiko viwili vya
mdalasini {vya chai}. Pakaa sehemu zilizoathirika usiku kwa muda wa
nusu saa, kisha safisha kwa sabuni na maji. Shida yako itakwisha
kwenye kipindi cha wiki moja.
4. Maamhukizo kwenye kihofu cha mkojo {BLADDER INFECTION}
Bilauri ya maji vuguvugu yaliyochanganywa na vijiko viwili {vya chai}
vya mdalasini na kijiko kimoja {cha chai} cha asali huondoa bacteria
kwenye kibofu. Unaweza ukatumia juisi ya cranberry badala ya maji
ikiwa ambukizo la kibofu linakuwa sugu.
5. Maumivu ya jino {TOOTHACHE}.
Changanya sehemu tano za asali, na sehemu moja ya mdalasini na tumia kwa maumivu ya jino.
Dondoshea kwenye jino au meno yaliyoathirika hadi maumivu yatakapotoweka.
6. Vidonda vitokanavyo kwa mgonjwa kulala kwa muda mrefu {CANKER
SORES}.
Saladi ya kupaka vidonda iliyochanganywa na asali pamoja na mdalasini
kwenye chai ya raspberry nyekundu ni dawa nzuri ya kuondoa maumivu
makali ya canker sores.
7. Helemu {CHOLESTERAL}
Kipimo cha helemu cha watu waliokuwa na afya nzuri {katika jaribio}
kilishuka kwa wastani wa asilimia 10 katika muda pungufu ya masaa
mawili baada ya kunywa bilauri moja {ounce 16} yenye vijiko viwili
vikubwa vya mdalasini iliyochanganywa na chai ya moto. Kinywaji hiki
kutwa mara tatu kilifanya kazi nzuri ya kushusha kiwango cha helemu
mwilini.
Madhara yaletwayo na vyakula vyenye mafuta yanaweza kudhbitiwa kwa
matumizi ya mara kwa mara ya chai hii pamoja na chakula chako. Hii
imeripotiwa na mtafiti maarufu Dr Alexander Andreyed na Eric
Vogelmann.
Ugunduzi wao uliyakinishwa kwenye jarida mashuhuri la kitiba la Denmark
July 1994. vilevile/ aidha uchunguzi mwingine ulibayanishwa kutoa
matumizi ya kila siku ya asali safi hupunguza viwango vya helemu.
8. Mafua {COLDS}
Mafua yameshaeleweka ya kwamba hupotea/huondoka baada ya masaa machache
baada ya waathirika kutumia kijiko kimoja {cha mezani} cha asali
vuguvugu iliyochanganywa na robo kijiko{cha chai} cha mdalasini,
mchanganyiko huu ni mahususi katika kusaidia kuondoa chafya na kuvimba
koo.
9. Ugumba {INFERTILITY}
Asali inaaminika kuamsha nyege na wapenzi wa jinsia zote mbili
wanashauriwa kunywa angalau vijiko viwili {vya mezani} kila siku kabla
ya muda wa kulala {usiku}.
Mdalasini umetumika kwa muda mrefu kwenye dawa za kihindi na kichina ili
kuongeza uwezo wa uzazi ka kina mama wenye kuhitaji kuzaa.
Kiungo hiki {mdalasini} huchanganywa na kiasi cha asali na kufanya
mgando {paste} ambao hupakwa kwenye fizi za meno na kunyonywa na
kuingia mwilini taratibu.
Familia moja iliyokuwa haina watoto iltumia mgando huu kwa mafanikio na
kupata mapacha wa kike baada ya kushindwa kwa muda wa miaka 14 kupata
mtoto. Walikuwa wameshakata tamaa ya kupata mtoto hadi waliposikia
kuhusu mchanganyiko huu wa asali na mdalasini.
10.Mchafuko wa tumbo {UPSET STOMACH}
Asali imetambuliwa kwa kipindi kirefu kama dawa ifaayo kuondoa mchafuko
wa tumbo pamoja na kichefuchefu. Ongeza kiasi kidogo cha mdalasini na
hii tiba ya kimaajabu vilevile itapunguza maumivu yaletwayo na vidonda
vya tumbo.
11. Esidi/Gesi-Co2. HCO3. HCl.
Kula
asali pamoja na mdalasini huweza kuondoa mchafuko wa tumbo na utumbo
uletwao na gesi/asidi kwa mujibu wa uchunguzi mahsusi iliofanywa huko
India na Japan.
12.Ugonjwa wa Moyo {HEART DISEASE}
Unaweza kukinga kupata ugonjwa wa moyo na kuzuia mkusanyiko wa mtandao
wa mafuta kwenye mishipa ya damu kwa kula asali na mdalasini mara kwa
mara-kwa kupakaa wakati wa kifiingua kinywa.
Kula asali ya mkate wa ngano yenye nyuzinyuzi nyingi iliyopakwa kijiko
kimoja {cha mezani} cha mchanganyiko huo hapo juu kila siku. Tiba hii
ya maajabu iliweza kupunguza kuganda kwa mishipa ya damu kwa 74% ya
wagonjwa waliokuwa katika nyumba za kutunzia wagonjwa - utafiti mmoja
ulionyesha.
13. Shinikizo la damu {HIGH BLOOD PRESSURE}
Shinikizo la damu pamoja na matatizo yaambatanayo ya maumivu ya kifua na
kizunguzungu yalitoweka kutoka kwa wagonjwa wengi wiki chache tu
baada ya watafiti wa kitaliano kuwapa dozi za mara kwa mara za asali
ilyochanganywa na mdalasini.
Vipimo vya shinikizo la damu vilionyesha ukawaida na wote 137
waliofanyiwa jaribio hilo waliripoti kujisikia vyema/vizuri baada ya
wiki chache za tiba hii ya ajabu.
14.Kinga ya mwili {IMMUNE SYSTEM}
Kinga yako ya mwili itaongezeka mara tatu zaidi ikiwa utatumia mara kwa
mara asali na mdalasini kwa pamoja - wataalamu wanasema.
Utafiti wa kitiba unaonyesha kwamba hazina kubwa ya
vitamini{vivurutubisho}na madini pamoja na michanganyiko mingine
iondoayo magonjwa pamoja na kinga itolewayo na chembechembe nyeupe za
damu, husaidia kuzuia magonjwa pamoja na kuharibu vimelea {virus} na
{bacteria}.
15.Ukosefu wa nguvu za kiume [Uhanithi]{IMPOTENCE}
Asali ina historia ndefu ya kuamsha uume pamoja na kuwa dawa madhubuti ya kuponyesha uhanithi.
Kutokana na uwezo wake kama kiamshaji/chaji, asali ilipigwa marufuku kwa
makasisi katika baadhi ya dini za kimashariki mwa Dunia. Mwaka jana,
watafiti wa kiaustralia waligundua kwamba asali ina uwezo wa kupeleka
mwili kutoa homoni mbalimbali kama ilivyo kwa mdalasini, katika Africa
na dunia ya kusini, mabaharia wamekuwa wakipaka asali katika sehemu
zao za nje ya uume ili kuongeza stamina zao za kufanya mapenzi.
16.Kutokuchaguliwa kwa chakula {INDIGESTION}
Vijiko viwili vya asali iliyonyunyiziwa mdalasini kabla ya mlo{kula
chakula} huondoa kiungulia na wataalamu wanasema kwamba asali husaidia
kutolewa kwa juisi zinazotumika kuchaguliwa kwa vyakula tumboni na
mdalasini unaongeza spidi ya kuchaguliwa kwa vyakula.
17.Flu {INFLUENZA}
Tafiti moja ya kihispania imethibitisha kwamba aina ya dawa moja asilia
ya ajabu ambayo huharibu vairasi {vimelea} waletayo Flu.
18.Umri wa kuishi {LONGERVITY}
Unaweza kuishi kufikia hadi miaka 100 na kufurahia maisha ya afya na
madhubuti kwa kunywa kila siku kikombe baridi cha chai ya mdalasini na
asali. Kutengeneza kinywaji hiki kitamu, weka vijiko vine{vikubwa} vya
mdalasini katika vikombe vitatu vya maji na koroga kwa dakika 10.
kunywa robo kikombe kutwa mara tatu au nne na hivyo utakuwa na
kinywaji kingi.
19.Chunusi {PIMPLES}
Changanya vijiko vitatu vya asali pamoja na kijiko kimoja cha mdalasini na pakaa kwenye chunusi.
Uwezo wa asali wa kuua bacteria utaufanya uso wako kuwa kawaida katika muda wa wiki mbili.
20.Kuumwa na wadudu {kwa washawasha} wenye sumu
Pakaa asali na mdalasini moja kwa moja kwenye sehemu zilizoathirika na
rudia wakati mwasho unapokuathiri. Rudia tena hadi viuvimbe
vinatoweka.
21.Madhara ya ngozi {INFECTIONS}
Fanya kama ilivyoelekezwa hapo juu. Rudia kufanya hivyo hadi hali itakapokwisha.
22.Kupungua kwa uzito
Wawezakufurahia vyakula vyote unavyopenda, kuwa na afya nzuri na
kupunguza uzito wa mwili ambao hauhitajiki kwa kula chakula chenye
nguvu na ladha nzuri, kilichojaa vitu viwili muhimu vya asili ambavyo
ni asali na mdalasini.unachohitajika kufanya ni kuhakikisha unavitumia
vyote kwa kiasi katika mapishi yako. Vilevile, wataalamu wanasema
unaweza kuondoa mabonge ya uvimbe wa nyamanyama nje ya mwili kwa
kuanza siku yako kwa kutumia vijiko viwili vya asali iliyochanganywa
na kijiko kimoja cha mdalasini ndani ya bilauri ya maji vuguvugu.
Rudia mchanganyiko huu kabla ya kulala.
Wakati wa kipindi cha baridi kinapokaribia, ambacho kinaambatana na
mazoezi machache, kuongeza hivi vitu viwili vya asili katika chakula
ni muafaka. Pia kinywaji hiki vuguvugu kimeshahakikishwa na wataalamu
wa lishe kwamba hupunguza hamu ya kula pamoja na kuleta joto mwilini.
23.Sarakani {CANCER}
Utafiti uliomalizika karibuni huko Australia na Japan, umeonyesha kuwa
asali ina uwezo mkubwa katika tiba ya mgonjwa anayetumia madawa ya
kutibu sarakani.
Katika tafiti iliyofanywa kwa wagonjwa waliokuwa wanaugua kwa kiwango
kikubwa sarakani ya mifupa na tumbo, wale waliokuwa wakitumia kila
siku dozi za asali na mdalasini, walionyesha maradufu kupata nafuu
kuliko wale waliokuwa wakitumia wakitumia madawa ya sarakani pekee.
"Tuliwapa kijiko cha mdalasini na asali kutwa mara tatu kwa
mwezi".anasema Dr Hiroki Owatta. "Wengine waliendelea na milo ya
kawaida".
24.Uchovu {FATIGUE}
Upo ushahidi mpya kwamba sukari asilia zilizopo kwenye asali zina uwezo
wa kuongeza nishati mwilini. Zikitumika ipasavyo, sukari hizi zinaweza
kuwasaidia wazee na wengine wanaosumbuliwa na uchovu, wataalamu
wanapendekeza kuchauganya nusu kijiko cha asali katika nusu bilauri ya
maji, nyunyizia mdalasini na kunywa masaa mawili baada ya kuamka
asubuhi. "Kunywa tena saa 9 alasiri wakati nishati {nguvu}inapoanza
kushuka" anashauri Dr Milton Abbozza ambaye kazi zake kuhusu asali na
mdalasini kama kichocheo cha nishati mwilini zinatambulika kimataifa.
"katika wiki moja hii itajionyesha".
25.Kuvimba Nyayo {SORE FEET}
Chua asali na mdalasini vuguvugu katika {miguu}
Hi guyz, i a'm so proud to see this blog keep it up na Mungu akubariki inshaallah.
ReplyDelete