Kila Tiba kati ya zifuatazo ni yenye
kujitegemea.Chagua iliyo rahisi kwako.Isipokufaa ndipo uchague nyengine.
Sharti za tabibu
1.Anatakiwa awe anaswali swala tano kila
siku.2.Aache kumshirikisha Mwenyezi Mungu.3Asiwe mchawi.4.Awe anafunga suna
siku za Jumatatu na Alkhamis pamoja na masiku meupe.5.Awe anapenda kusimama
usiku katika ibada ya swala za usiku kama tahajjud.6.Awe anafanya uradi kila
siku na kuleta dua za kumuomba Mwenyezi Mungu ampe nguvu za kupambana na
majini.
Namna ya kumtoa jini katika mwili wa mwanadamu.
Kwanza tabibu atie udhu na kisha aombe
dua zifuatazo na baadae kumswalia Mtume mara mia moja wakati huo mgonjwa awe
amekaa chini.
Dua ya 1:Ayatul Qursiy mara 7.
Dua ya 2:Surat Dhaariyaat mara 3
Dua ya 3:Surat Ikhlaswi mara 3
Dua ya 4:Suratin Nnaas mara 3
Dua ya 5:Soma HASBUNA LLAAH WA NEEMAL
WAKEELmara 100 na kumalizia na Laa Haula wala Quwwata illa Bilaahil Adhwiim.
Utaratibu huu utarudiwa kila siku kwa
muda wa wiki 1.
No comments:
Post a Comment