FAIDA YA JUISI YA KABICHI KWA AFYA NA KUTIBU VIDONDA VYA TUMBO NA SARATANI
Vidonda vya tumbo
ni ugonjwa ambao umekuwa ukiwasumbua watu kadhaa na hata kusababisha
kifo kutokana na kuvidonda kuwa vikubwa, utumbo kuharibika, kupoteza
damu nyingi na kupatwa na saratani.
Mojawapo ya njia za asili
za kupambana na ugonjwa wa vidonda vya tumbo pamoja na aina fulani za
saratani kama vile sarafani ya korodani, matiti na utumbo mkubwa, ni kwa
kutumia juisi inayotengenezwa kutokana na kabichi. Walioitafiti
wanasema kabichi ina uwezo wa kupambana na asidi ya tumboni kwa kuwa ina
L-glutamine na gefarnate ambazo zinalinda ngozi laini ya viungo
vilivyotajwa hapo juu.
Juisi ya kabichi pia inawafaa
wanaopenda ngozi zao ziwe nyororo ikiwa wataichanganya kwa karoti ama
asali na hata hamira, kisha wakajipaka kwenye ngozi na kusubiri dakika
15 kabla ya kusafisha kwa maji.
Mahitaji:
Kabichi
ya ukubwa wa wastaniMaji safi na salama yaliyochemshwa na kuchujwa ili
kupunguza chumvi chumvi (au tumia distilled water)
Kisu cha kukatiaMahali pa kukatiaBlender ya kuchanganyaChupa yenye mfuniko kwa ajili ya kuhifadhiaChujio/chekeche
Kata kabichi na kujaza vikombe
vitatu Ongeza maji vikombe viwili kwenye kabichi iliyokatwaChemsha
mchanganyiko huo katika moto wa wastani kwa dakika 25 hadi nusu saa
hivi.Weka mchanganyiko wako huo kwenye blender (kama ni kubwa weka mara
moja, kama ni ndogo weka kidogo kidogo) kisha washa blender ifanye kazi
yake kulainisha kidogo tu kabichi ila isiwe rojo rojo.Mimina
mchanganyiko wako kwenye
chupa ya kuhifadhia na
kisha ifunike ili hewa isiingie ndani (ikibidi weka nailoni kwenye
mdomo wa chupa kabla ya kukaza kifuniko)Ihifadhi chupa hiyo kwenye
sehemu ya kawaida (room temperature, siyo kwenye jokofu/friji) na iache
itulie hivyo kwa siku kati ya 3 hadi 5 ili ichachuke
(fermentation). Hatua hii
inasaidia bakteria wenye manufaa (kama wanaochachusha maziwa
mgando/mtindi) kufanya kazi inayotakiwa vyema ili juisi iwe na nguvu
inayohitajika katika mfumo wa mmengenyo wa chakula, tumboni, utumbo
n.k.Siku ya tatu au ya nne ama ya tano, chukua kichujio (chekeche),
faneli (funnel) na chupa nyingine kisha chukua ile yenye mchanganyiko
uliouhifadhi, ifungue (itakuwa inatoa harufu
inayonuka kwa sababu ya kuchachuka),
kisha anza kuchuja kwa kumimina juisi iliyomo kwenda kwenye chupa isiyo
na kitu.Juisi yako ni tayari kunywewa na unaweza sasa kuihifadhi kwenye
jokofu/friji ipate ubaridi unaoutaka na vile vile kuzuia isiendelee
kuchachuka haraka zaidi kama awali.Makapi ya kabichi uliyochuja unaweza
kuyahifadhi kwa matumizi tena ya siku inayofuata kwa kuyaongezea kikombe
kimoja cha
mchanganyiko mpya na kuacha yakae
tena kwenye joto la kawaida (room temperature) kwa siku moja (kwa kuwa
tayari kiasi kikubwa kimeshachachuka) na kuyachuja siku inayofuatia ili
kupata juisi nyingine.
No comments:
Post a Comment